FAIDA ZA PAPAI
Papai ambao kitaalam hujulikana kama
Carica papaya, ni mti wenye tunda lenye virutubisho vingi ambao una
asili na hulimwa na kustawi katika nchi za kitropiki. Mpapai hukua hadi
kufikia kimo cha mita 10. Mti huu huwa na makovu ambayo hutokana na majani ya
mpapai yaliyoanguka unapokua.
Tunda la papai lililowiva lina
kiwango kikubwa cha Vitamini C (62mg) ukilinganisha na chungwa lenye kiwango
cha 53mg katika gramu 100 za tunda. Tafiti zimeonyesha faida nyingi za vitamini
C kama kuondoa sumu mwilini(sumu hizi hujulikana kama free radicals),
kuimarisha kinga ya mwili na kujikinga na visababishi vya maumivu na uvimbe.
Papai hupunguza kiwango cha lehemu
kwa kuwa lina Vitamini C na virutubisho vingine ambavyo huzuia kujijenga kwa
lehemu katika mishipa ya damu ya ateri. Lehemu inapojikusanya kwa wingi
katika ateri, mishipa hii ya damu huwa na njia nyembamba au kuziba na
kusababisha kuongezeka shinikizo la damu na hata shambulizi la moyo.
Tunda hili husaidia kupunguza uzito
wa mwili, papai lina fiba (nyuzi lishe) ambazo husaidia kupunguza uzito,
unapokula tunda hili, fiba husababisha kujisikia umeshiba kwa hiyo mtu
hupunguza kiasi cha chakula chenye nishati nyingi ambapo hupelekea kupunguza
uzito wa mwili.
Afya njema ya macho hupatikana kwa
kula tunda hili. Papai lina kiwango kikubwa cha Vitamini A na vitutubisho
vingine kama Beta carotene ambavyo husaidia kuiweka katika hali ya afya
njema ya ngozi utando ya macho, na kuzuia kudhurika kwa macho. Pia vitamini A
huzuia kuharibika sehemu ya macho inayohusika na kuona kutokana na umri mkubwa
na kutuepusha matatizo ya kuona.
Papai
husaidia kuboresha mmeng'enyo, katika zama hizi, haikwepeki kula vyakula
ambavyo huathiri mmeng'enyo na mfumo wa chakula. Mfano tunapokula vyakula
vyenye mafuta na chumvi kwa wingi katika migahawa (junk food). Kula
papai kutarekebisha mfumo kutokana na kuwepo kwa kimeng'enyo kijulikanacho
kama papain pamoja na fiba kwa wingi ambazo husaidia kuboresha
mmeng'enyo na kuimarisha afya yako
No comments