FAIDA ZA PARACHICHI
Parachichi ni tunda la pekee ukilinganisha na matunda mengine, kimsingi matunda mengine huwa yana wanga(carbohydrate) kwa wingi, wakati parachichi lina aina ya mafuta ambayo yana faida kwa afya.
Parachichi ni tunda la pekee
ukilinganisha na matunda mengine, kimsingi matunda mengine huwa yana wanga(carbohydrate)
kwa wingi, wakati parachichi lina aina ya mafuta ambayo yana faida kwa afya.
FAIDA ZA PARACHICHI
Hupunguza lehemu mbaya (cholesterol)
Mafuta
ya lehemu ni hatari ikiwa kiwango chake kitakuwa kingi mwilini; mafuta haya
husababisha matatizo mbalimbali hasa maradhi ya moyo.
Matunda
ya parachichi hayana lehemu mbaya inayoweza kuathiri afya yako. Utafiti
unaonyesha kuwa watu wanaokula parachichi kiwango chao cha lehemu mwilini ni
tofauti na wale wasiokula kabisa.
Kukabili maradhi ya kisukari
Parachichi ni tunda ambalo kiwango chake cha
sukari hakina athari kwenye mwili. Hivyo utumiaji wa parachichi utakuwezesha
kuweka kiwango cha sukari mwilini kuwa katika hali nzuri ya wastani.
Hulinda afya ya moyo
Madini ya potasiamu yanayopatikana kwenye tunda
la parachichi kwa zaidi ya asilimia 14 ni muhimu sana katika utendaji kazi wa
misuli ya moyo.
Hulinda afya ya macho
Kemikali ya lutein na zeaxanthin ni muhimu sana
kwa ajili ya kulinda na kuimarisha afya ya macho.
Ikumbukwe kuwa parachichi ni tunda lenye kiasi
kikubwa cha lutein ambayo pia hulinda macho dhidi ya matatizo mbalimbali
yatokanayo na umri.
Parachichi lina Potasiamu nyingi kuliko ndizi
Watu wengi wanapenda ndizi kwa kuwa ni chanzo
kimoja wapo cha madini ya potasiamu, lakini hawafahamu kuwa ndizi ina potasiamu
asilimia 10 na parachichi lina asilimia 14. Hivyo parachichi ni bora zaidi.
Potasiamu ni muhimu katika miili yetu kwani
hutuwezesha kutawala kiwango cha sodiamu katika miili yetu na kutuepusha na
madhara yatokanayo na madini haya ya sodiamu.
Huboresha afya ya nywele na ngozi
Naamini umewahi kusikia kuwa parachichi hutumika
kutengenezea mafuta ya nywele na ya ngozi; hii ni kutokana na kusheheni
vitamini E ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya ya nywele na ngozi zetu.
Huzuia saratani
Tafiti zilizofanyika zimebainisha kuwa kula
matunda ya parachichi kunasaidia kupunguza kasi ya ukuaji wa seli za saratani
ya tezi dume.
Hata hivyo, tafiti juu ya swala hili siyo nyingi
sana lakini bado unaweza kula parachichi na kupata faida nyingine kemkem.
Huimarisha mifupa
Kutokana na parachichi kuwa na vitamini K pamoja
na madini ya kopa na folate ambavyo ni muhimu kwa ajili ya mifupa, tunda hili
linakuwa na nafasi kubwa katika kuimarisha mifupa.
Huboresha mmeng’enyo wa chakula
Vyakula vyenye nyuzinyuzi ni muhimu sana kwa
ajili ya kuufanya mmeng’enyo wa chakula uende vizuri. Parachichi ni tunda lenye
nyuzinyuzi kwa karibu asilimia 13 ambazo ni sawa na kiwango cha asilimia 54
unachotakiwa kula. Je bado huoni umuhimu wa tunda hili? Anza kula ili uboreshe
mmeng’enyo wako wa chakula sasa.
Ni muhimu kwa wajawazito
Kuwepo kwa kiasi kikubwa cha folate, potasiamu,
Vitamini C na B6 ambazo ni muhimu kwa ajili ya afya na ukuaji wa mtoto;
kunalifanya tunda la parachichi kuwa na umuhimu mkubwa kwa wajawazito.
Hivyo inashauriwa wanawake wajawazito wazingatie
ulaji wa matunda hasa tunda la parachichi.
Huimarisha kinga ya mwili
Kinga ya mwili hutegemea vitamini B, C na E ili
kujiimarisha na kujijenga. Hivyo ulaji wa parachichi utaimarisha kinga ya mwili
yako kwani parachichi limesheheni vitamini B, C na E.
Huboresha afya ya ubongo
Madini ya kopa yanayopatikana kwenye parachichi
kwa zaidi ya asilimia 19 yana nafasi kubwa sana katika kuufanya ubongo ufanye
kazi vyema.
Hivyo basi, ukitaka kuweka afya ya ubongo wako
katika hali nzuri na kuweza kufikiri vyema, basi kula tunda la parachichi mara
kwa mara.
No comments