UTAPIAMLO
SEHEMU YA KWANZA
hali ya afya na lishe bora kwa mama mjamzito ni muhimu kabla
na baada ya ujauzito kwa kuwa husaidia kuwepo kwa matokeo mazuri ya ujauzito na
kufanikisha unyonyeshaji wa maziwa ya mama.
Ndani ya siku 1000 yani
tangu mama apate ujauzito hadi mtoto anapofikisha umri wa miaka miwili ni
muhimu akazingatia lishe bora pamoja na mtoto wake ili kuhakikisha mtoto anakua
vizuri na kuepuka matatizo ambayo anaweza kuyapata ikiwemo utapiamlo, ugonjwa
unaotokana na kupunguza au kuzidisha mahitsaji muhimu katika mwili.
Kuna aina mbalimbali za
utapiamlo ambazo mtoto anaweza kuzipata ikiwemo utapiamlo wa kukonda, utapiamlo
wa ufupi na hali hiyo huwa hivyo mpaka kwenye maendeleo ya ubongo wake.
Mtoto kuwa na uzito
usioendana na umri na utapiamlo wa madini na vitamini ambao unaweza
kuwapata hata watoto warefu na kwamba una dumaza ubongo wa mtoto.
“Unaweza kumkuta mtu mrefu
lakini amekuwa na shida katika uelewa wake kwakuwa anakuwa na uelewa wa hali ya
chini sana”,anasema Mary.
Utapiamlo usababishwa na
mambo mbalimbali ikiwemo ukosefu wa chakula, hali ya usafi wa chakula,
kutokuwepo kwa uangalizi na kwamba zipo sababu zilizojificha ambazo ni pamoja
na umaskini unaobabisha kukosa chakula, uwezo wa mama kufanya maamuzi na
mazingira ya njaa na hivyo waathirika wakuu ni watoto walio chini ya umri wa
miaka miwili na kina mama.
Mary alieleza kuwa madhara
ya utapiamlo kuwa ni pamoja na vifo vya watoto 130 kila siku, huaribu mfumo wa
kinga mwili na kusababisha maradhi, watoto waliozaliwa na uzito pungufu hupata
kisukari, hupata matatizo ya moyo, kuwa na uwezo mdogo na kukosa uwezo wa
kuzalisha na kufanya maamuzi.
Binafsi nimeshuhudia baadhi
ya watoto waliopata utapiamlo kutokana na kutozingatia taratibu za lishe ambazo
mzazi ama mlezi anatakiwa kuzifuata ikiwa pamoja na wazazi wenyewe kuwa na afya
duni, hali inayoweza kusababishwa na mambo mbalimbali yanayomkwamisha
mama kupata lishe bora kwake na mtoto wake.
CONTACTS
0714959285/0683879783
No comments