LISHE KWA MTU MWENYE KISUKARI
Ugonjwa wa kisukari ni tatizo ambalo siku hizi
husababishwa na mfumo wa maisha tunayoishi hasa vijana, tafiti zilizowahi
kufanywa zinaonesha kuwa vijana wapo kwenye hatari kubwa ya kupata kisukari kwa
sababu ya mfumo usio sahihi wa maisha wanayoishi vijana.
Kutokufanya mazoezi, kukosa muda wa kupumzika na kutokula
mlo sahihi,unywaji wa pombe na uvutaji sigara wa kupitiliza, hizi ni sababu
chache zinazochangia vijana kuishi katika mfumo wa maisha hatarishi wa kupata
maradhi ya kisukari.
Leo tunaangalia suala zima
la chakula kwa watu mwenye maradhi ya kisukari,madaktari wapo wengi sana kwenye
hospitali zetu pamoja na majumbani mwetu lakini wewe mwenye ugonjwa wa
kisukari ndiyo daktari namba moja katika kutibu afya yako.
Kitu muhimu kwa mgonjwa wa
kisukari ni kufahamu ya kwamba ana uwanja mpana sana wa
vyakula anavyoruhusiwa kula tofauti na na mazoea yaliyojengeka miongoni
mwetu kuwa mtu anayeuugua maradhi haya basi ana vyakula vyake vya kipekee
kabisa. Maisha ya mtu mwenye kisukari yanatakiwa kuendelea kama kawaida, na
unaruhusiwa kula aina zote za vyakula isipokuwa tu vile venye sukari.
Unakula kile kilichopo na
kinachokuwepo na usijiulize ule nini ila jiulize ule vipi hicho
chakula kilichopo,kwa mfano, nyumbani kuna pilau, usipoteze muda na kusema mimi
nina kisukari kwa hiyo siwezi kula pilau,la hasha. Kitu unachotakiwa
kujua ni ule vipi hiyo pilau. Pilau ni chakula chenye wanga,na kwa kuwa vyakula
vya wanga kazi yake ni kutengeneza nishati mwilini kwa maana hiyo wanga
utengeneza sukari, na tayari wewe una kisukari, basi hautakiwi ule wanga
mwingi, sasa hapa cha kufanya ni kula kiasi kidogo cha pilau ili kuepuka
utengenezwaji mwingi wa sukari mwilini.
Upawa mmoja tu wa
pilau,nyama kidogo na mboga za majani au kachumbari kwa wingi na hivyo
ndiyo unavyotakiwa kula kila mlo wako, hakikisha unakula kiasi kidogo cha
wanga, na kiasi kikubwa au kingi cha mboga za majani.
AFYA BORA INATOKANA NA LISHE BORA
CONTACTS: 0714959285
No comments