Carousel

Breaking News

UZITO WA MWILI UNAOPASWA KUWA NAO KULINGANA NA UREFU WAKO





 Katika hali ambayo ni mazoea watu wengi tumekuwa tukitamani na kujitahidi kuwa na mwili wenye umbo au uzito fulani.Hii imekuwa ikifanyika kwa kujiwekea mipaka katika ulaji wa vyakula na pia hata kujihusisha na aina mbalimbali za mazoezi.
Kwa mujibu wa hesabu wa kiafya au kitaalamu uzito wa mwili hutegemeana na urefu wa mtu ambayo kuna kanuni kitaalamu huwezesha kujua mtu mwenye urefu fulani anatakiwa awe na uzito gan? kanuni hiyo ambayo hujulikana kama BMI (BODY MASS INDEX) hutupatia uwiano wa uzito wa mwili na urefu wake

BMI = uzito wa mwili katika kilogramu(kg)/ urefu katika mita za mraba(M^2) kutokana na kanuni hiyo ukichukuia uzito wa mwili katika vipimo vya kilogramu ugawanya na urefu wa mwili wako katilka vipimo nvya mita utapata namba ambayo kitaalamu itakuwezesha kujua kama uzito wa mwili wako upo sawa

Mchanganuo wa namba unaweza kuupata baada ya kugawanya uzito wako na urefu wako ni kama ifuatavyo

Chini ya 18.5 mtu huyo ana uzito pungufu( underweight)
Kuanzia 18.5-24.5 uzito wa kawaida ambao kiafya ni salama(normal weight)
Kuanzia 25-29.5 uzito mkubwa ( overweight)
Kuanzia 30 n kuendelea ni uzito uliokithiri (obesity)


CONTACTS
0714959285
0683879783

No comments