LISHE BORA KWA MTOTO MIEZI 6 NA KUENDELEA
VIRUTUBISHO MUHIMU KWA MTOTO WA MIEZI 6 NA KUENDELEA
wanga
- kuupa mwili nguvu eg.mahindi/mchele
- hujenga mwili eg. soya/maharage/samaki
- kuupa mwili joto eg.ufuta/karanga
- kulinda mwili dhidi ya magonjwa eg. mboga za majani
JINSI YA KUANDAA UJI WA LISHE BORA KWA MTOTO
Mahitaji
- Mahindi ya njano-1kg
- Ulezi-robo kilo
- Soya-nusu kilo
- Ufuta-robo kilo
UCHANGANYAJI
- Osha mahindi ,ulezi, soya na ufuta vizuri kila mmoja peke ake baada ya kuchambua
- anika kuani hakikisha vumbi halitaingia
- changanya vyanzo vyako na kisha saga
- unga tayari kwa matumizi
Ni muhimu kuhakikisha umetoa maganda ya soya vizuri baada ya kuweka kwenye maji ya moto ili iwe rahisi kutoa maganda baada ya hapo unaanika juani zikauke vizuri na hatua inayofuata ni kuzikaanga vizuri na tunatoa maganda ili kuruhusu unyonywaji wa virutubishi vya protini katika mwili wa mtoto.
NYONGEZA
Tunashauri pia uwekaji wa karanga kama unaandaa lishe ya unga kwa mda mfupi kwa sababu karanga ni rahisi kuharibika zikakaa mda mrefu zaidi ya wiki inaweza kumletea mtoto madhara kama kuharisha
UPIKAJI
Hakikisha unapika uji kwa mda usiopungua nusu saa na kuendelea ila hakikisha unaiva vizuri
No comments