NJIA RAHISI NA SALAMA YA KUPUNGUZA TUMBO
Njia iliyosalama ya kupunguza mafuta katika tumbo au kupunguza tumbo kubwa ni ile ya kupangilia chakula na kufanya mazoezi.
Kama unataka kupunguza tumbo kwa haraka basi punguza kula vyakula vyenye wanga na badala yake tumia mbogamboga na matunda kwa wingi. Vyakula kama viazi mviringo, wali mkate hukaa tumboni kwa zaidi ya siku tatu, pia ulaji wa nyama nyekundu inasababisha kuongezeka uzito na pia huongeza ukubwa wa tumbo,vyakula hivyo vinatakiwa kutumiwa kwa kiasi kidogo sana
Kama mtu anataka kupunguza mafuta au kuondoa kitambi anatakuwa kula milo mitatu kwa siku na si kujinyima kula kwa kudhani kuwa unaweza kupungua uzito
Vyakula vya wanga na mafuta ufanya mtu kunenepa, acha au kupunza kula vyakula vyenye wanga ili kupunguza mafuta yaliyozidi mwilini, mafuta yanaporundikana mwilini athari moja kubwa ni kuwa na tumbo kubwa
Tumbo kuwa kubwa ni dhahiri kuwa chakula unachokula hakifanyi kazi inayotakiwa, kumekuwa na ziada mwilini na hii ziada inafanyika mafuta ambayo hujiwekesha akiba katika maeneo mbalimbali ya mwili
Asubuhi pata kifungua kinywa kilichokamilika, pata mlo wa mchana kama kawaida na usiku kula matunda tu kunaweza kufanya mwili wako uwe katika hali inayotakiwa.watu wengi wanatumia wanga mwingi wakati wa usiku muda ambao unaenda kulala na ziada ya chakula haifanyi kazi vizuri zaidi ya kujikusanya, kujibadilisha na kuhifadhiwa katika maeneo mbalimbali ya mwili hasa tumboni.
Mazoezi husaidia kupunguza uzito wa mwili na manyama uzembe? Mazoezi ya viungo yamethibitishwa kusaidia kuchoma mafuta ya ziada katika mwili.
Unapofanya mazoezi ya viungo unaongeza hewa ya oksijeni kwa wingi katika mapafu yako na wakati huohuo mwili nao unaunguza mafuta ili kutoa nguvu kwa mwili. Mafuta yanayounguzwa kwanza ni yale ya kawaida kabla ya kuingia katika akiba. kuna umuhimu wa kutambua kuwa mazoezi ni kitu cha bure na kama ukifanya kwa mpangilio yanasaidia kupunguza maunyama uzembe tumboni.
No comments