Carousel

Breaking News

JIFUNZE KUHUSU LISHE BORA




Lishe bora ni lazima kwa watoto wadogo kwa sababu wanatakiwa kukua vizuri kimwili na kiakili. Karibu twende sawa wewe unaesoma makala hii iliyoandaliwa kwa ajili yako ili upate kufahamu kama unakula chakula bora ama bora chakula?
JE LISHE BORA NI IPI?
Lishe bora ni cha kula chenye virutubisho vyote kwa kiasi na uwiano sahihi ili kuuwezesha mwili wa mtoto kupata siha zuri au afya bora. Lishe bora inatakiwa kuwa na mboga za majani ,matunda,ptotini,madini,wanga na maji na hizi zinapatikana kwenye vyakula aina tofauti  na vyakula vingine vinavirubishi vingi kwa pamoja.
kwa mfano vyakula vyenye lishe bora kwa kiwango kinachofaa ni kama mboga za majani,mtunda ,nafaka asilia,vyakula vya protini(mayai,maharage,nyama n.k) na vyakula vyenye mafuta yasiyoifadhiwa mwilini.

Watoto wanagawanywa kwenye makundi ya aina mbili; kuzaliwa hadi miezi 6 na kuanzia miezi 6 na kuendelea.Haya makundi ni muhimu  kwa sababu watoto waliopo kwenye makundi  haya wanatofautiana aina ya vyakula wanavyokula.Ni muhimu kuzingatia hili sababu huu ndo mda  muhimu zaidi katika ukuaji wa mtoto.

LISHE YA MTOTO MCHANGA HADI MIEZI 6
inashauriwa kwamba mtoto mchanga tangu anazaliwa mpaka afilishapo miezi 6 asipewe kitu chochote zaidi ya maziwa ya mama,hii ikiwa inamaanisha hata maji ya kunywa maziwa ya mama yana virutubisho vyote muhimu( pamoja na maji) na vinavyohitajika kwa ukuaji mzuri wa mtoto na kumpa kinga ya magonjwa mbalimbali.



LISHE YA MTOTO KUANZIA MIEZI 6

Mtoto akishafika umri wa miezi 6, anaweza kuanza kula vyakula mbalimbali. Inashauriwa mtoto aanze kupewa vyakula mbalimbali kidogo kidogo ili apate kuzoea. Vyakula hivi lazima viwe vimepondwa, au viwe kwenye mfumo wa uji au maji sababu mtoto anakuwa hana meno yaliyokomaa au wengine wanakuwa hawajaanza kabisa kuota meno.

LISHE YA MAMA





Ukizungumzia mtoto hutoweza kuacha kuzungumzia mama. Mama ndiyo chanzo kikubwa cha chakula kwa mtoto tangu anazaliwa hadi anakuwa huru kula chakula cha kawaida. Kwa mwanamke mwenye umri wa kubeba ujauzito au mwenye ujauzito, ni muhimu kula vizuri ili kujenga afya ambayo ndio chanzo kikubwa cha virutubisho kwa mtoto tumboni na baada ya kuzaliwa. Ili kuwa na siha nzuri, vyakula vyote vinatakiwa kuwa na uwiano mzuri wa virutubisho.


Inatakiwa kuzingatiwa kuwa, vyakula vya mtoto viwe vya kuongezea lishe, lakini ni vizuri mtoto akiendelea kunyonya maziwa ya mama hadi atakapofikisha miezi 24. Maziwa ya mama ni muhimu katika kumfanya mtoto akue vizuri, hasa katika miezi 24 ya mwanzo. Inashauriwa kuwa, kama hakuna kikwazo mfano: ugonjwa wa maambukizi unaoweza kumdhuru mtoto ni vizuri mama amnyonyeshe mtoto kwa muda mrefu zaidi ya miezi sita (6).

Faida kubwa ya kunyonyesha ni kusaidia ubongo wa mtoto kukua vizuri zaidi sababu maziwa ya mama yanatoa virutubisho kwa wingi kuliko vyakula atakavyokula yeye moja kwa moja. Hii ni kwa sababu, tumbo la mtoto linakuwa halijazoea kusaga vyakula tofauti, hivyo maziwa ni chakula kinacholeta virutubisho vinavyotumika moja kwa moja mwilini.



 

        




No comments